Mkaguzi wa Ndani Bwn. Imani Bukuru toka Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru akisoma taarifa ya ukaguzi wa Wilaya, katika kikao maalum cha baraza la madiwani wa kupitia ripoti ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali pamoja na hoja za ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Mtaalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mhandisi Ramadhani Magaila akielezea jinsi mradi utakavyokuwa katika kijiji cha Mbati.
Katika hatua kubwa ya kuimarisha sekta ya kilimo na kuongeza uzalishaji wa chakula, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeidhinisha kuanza kwa mradi mkubwa wa umwagiliaji katika Kijiji cha Nambarapi, Kata ya Masonya, Wilaya ya Tunduru. Mkandarasi aliyepewa dhamana ya kutekeleza mradi huu ataanza kazi tarehe 29.07.2024, na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 18, kufikia tarehe 31 Desemba, 2025.
Makabidhiano ya mradi huu wenye thamani ya shilingi bilioni 6,314,477,066.00 baina ya Tume ya Taifa ya umwagiliaji kwa mkandarasi yamefanyika kwa sherehe za hadhara katika kijiji cha Nambarapi, zimehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Simon Chacha, ambaye alikuwa akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed.
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.