• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Departiment
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Msingi
      • Maji
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maliasili na Utalii
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utumishi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Information, Technology, Communication and Public Relation
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Kilimo
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
      • Kata ya Mbati
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

Elimu Sekondari

Elimu Sekondari

    

UTANGULIZI

Idara ya Elimu ya Sekondari ni moja ya idara za Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru. Idara hii ilianzishwa mwaka 2009 baada ya  Serikali kugatua usimamizi na uendeshaji wa shule za sekondari kutoka kwenye Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwenda  na kusimamiwa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa (Halmashauri za Wilaya/Miji/Manispaa/Majiji).


Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru  ina Jumla ya shule za sekondari 23, kati ya hizo shule 21 ni za Serikali na shule 2 ni za mashirika ya Dini.Shule hizi 21 za serikali ni za kutwa na bweni kwa wanafunzi, na jumla ya shule 4 kati ya 21 za serikali zinapokea wanafunzi wa kidato cha tano na sita.

2.     DIRA NA MWELEKEO


2.1    DIRA, DHIMA NA MALENGO YA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA 2014


Msingi wa elimu na mafunzo utajikita katika kumjengea Mtanzania misingi bora ya malezi, maadili, ujuzi,umahiri na kumwezesha kujitegemea. Elimu ya kujitegemea itaendelea kuongoza utoaji wa elimu na mafunzo kwa kuzingatia mabadiliko yanayotokea katika jamii, kisiasa, kiuchumi, kisayansi na kiteknolojia.


2.1.1 DIRA


Kuwa na Mtanzania aliyeelimika na mwenye maarifa, stadi, umahiri, uwezo na mitazamo chanya ili kuweza kuchangia katika kuleta maendeleo ya Taifa.


2.1.2 DHIMA


Kuinua ubora wa elimu na mafunzo na kuweka mifumo na taratibu zitakazowezesha kupata idadi kubwa ya Watanzania walioelimika na wanaopenda kujielimisha zaidi ili waweze kuchangia katika kufikia malengo ya maendeleo ya Taifa letu.


2.2    LENGO LA JUMLA LA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO


Kuwa na Watanzania walioelimika na wenye maarifa na ujuzi kuweza kuchangia kwa haraka katika maendeleo ya Taifa na kuhimili ushindani.


3.     ELIMU YA SEKONDARI


3.1    MATAMKO YA SERA KUHUSU ELIMU YA SEKONDARI


3.1.1 SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 1995


Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 ilifafanua kuwe Elimu ya Sekondari ina maana ya  Programu (Mpango)  kamili wa elimu inayotolewa kulingana na Mitaala ya Serikali na kupatikana kwa wanafunzi ambao watakuwa wamemaliza elimu ya msingi.


Nchini Tanzania elimu rasmi ya shule za Sekondari ina ngazi mbili. Ngazi ya kwanza ni elimu ya sekondari ya Ngazi ya Kawaida  ya miaka  minne, ambapo ngazi ya pili ni Programu ya Miaka miwili ya elimu ya Sekondari ya ngazi ya Juu. Ngazi ya kawaida huanzia kidato cha I na kuishia kidato cha 4, wakati Ngazi ya Juu ina kidato cha 5 mpaka cha 6


3.1.2         SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014


Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 imerekebisha muda wa elimu na mafunzo katika ngazi mbalimbali ili kuleta tija, ufanisi na matumizi bora ya rasilimali


                TAMKO


3.1.2.1      Serikali itaweka utaratibu wa elimu ya awali kuwa ya lazima na kutolewa kwa watoto wenye umri kati ya miaka mitatu hadi mitano kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja.


3.1.2.2      Serikali itaweka utaratibu wa elimumsingi kuwa ya lazima kuanzia darasa la kwanza hadi kidato ha nne; na kutolewa kwa miaka kumi na umri wa kwanza darasa la kwanza kuwa kati ya miaka minne hadi sita kulingana na maendeleo na uwezo wa mtoto kumudu masomo katika ngazi husika.


3.1.2.3      Serikali itaweka utaratibu wa kuhakikisha muda wa kukamilisha elimu na mafunzo katika ngazi mbalimbali za elimu baada ya elimumsingi unalenga mwanafunzi kupata ujuzi stahiki kulingana na Mfumo wa Tuzo wa Taifa.


3.1.2.4      Serikali itahakikisha kuwa elimumsingi katika mfumo wa umma inatolewa bila ada.


4.     LENGO LA IDARA


Kutoa nafasi ya upataji maarifa, ujuzi na kuelewa ili wanafunzi wajiunge na taasisi za ufundi na mafunzo ya kitaalamu ya elimu ya juu.


5.     VITENGO VILIVYOPO KATIKA IDARA


Idara ya elimu ya sekondari ina jumla ya vitengo viwili (3) ambavyo hufanya shughuli zake kwa ushirikiano na kumsaidia mkuu wa idara ambaye ni msimamizi mkuu wa shughuli za idara katika kuleta matokeo tarajiwa.  Vitengo vya idara ni pamoja na kitengo cha Taaluma kinachosimamiwa na Afisa Elimu Taaluma Wilaya,  kitengo cha Vifaa na Takwimu kinachosimamiwa na Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Wilaya na kitengo cha ufundi kinachosimamiwa  na Afisa Ufundi wa Wilaya na   vyote vikiwa chini ya mkuu wa idara ambaye ni Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya.


5.1   MAJUKUMU YA VITENGO


5.1.1        MAJUKUMU YA AFISA ELIMU TAALUMA (W)


Kusimamia masuala yahusuyo maendeleo ya taaluma na michezo katika shule za sekondari wilayani.


5.1.2        MAJUKUMU YA AFISA ELIMU VIFAA NA TAKWIMU (W)


Kukusanya kuchambua na kuunganisha  takwimu mbalimbali zinazohusu elimu ya sekondari.


5.1.3        MAJUKUMU YA AFISA ELIMU UFUNDI


Kusimamia upanuzi wa elimu ya sekondari kusimamia ujenzi wa  majengo mapya katika shule za zamani au katika kuanzisha Shule mpya.

kwa tarifa zaidi bofya hapa

Matangazo

  • KUITWA KAZINI TUNDURU DC July 09, 2022
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2022- 2023 January 04, 2023
  • Watumishi wa Umma walioma mwezi julai August 12, 2018
  • Orodha ya majina ya wanafunzi waliopangiwa kidato cha tano mwaka 2019 June 02, 2019
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • Pongezi kwa Dc Mtatiro

    January 26, 2023
  • Makusanyo Robo ya 1&2 Tunduru Dc Bilioni 2.5 Sawa na 54%

    January 26, 2023
  • BILIONI 26.7 ZAINGIA KWENYE MZUNGUKO KUPITIA ZAO LA KOROSHO

    January 19, 2023
  • Makabidhiano ya Gari Isuzu Tani 7 kati ya Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkurugenzi wa TAMESA

    January 18, 2023
  • Ona Zote

Video

KILO 1,147,287 ZA KOROSHO ZIMEUZWA KWENYE MNADA WA SABA TUNDURU DC
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Taarifa ya Ukimwi kuishia decemba 2017
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.