• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Departiment
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Msingi
      • Maji
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maliasili na Utalii
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utumishi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Information, Technology, Communication and Public Relation
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Kilimo
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
      • Kata ya Mbati
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

Usafi na Mazingira

IFAHAMU IDARA YA MAZINGIRA NA UTHIBITI WA TAKA NGUMU



Jonathan Albano Haule

Mkuu wa Idara

Idara ya Mazingira na Uthibiti wa Taka Ngumu ni mojawapo ya idara katika Halmashauri ya wilaya ya Tunduru, Idara ina mtumishi mmoja tu, ambaye kwa sasa ndio Mkuu wa Idara.

 

Majukumu ya Idara:

- Kukusanya takwimu na taarifa mbalimbali zinazohusu usimamizi na hifadhi ya mazingira

- Kutoa elimu ya hifadhi ya mazingira kwa wadau mbalimbali

- Kushiriki katika kuandaa mpango kazi na bajeti za idara

- Kushiriki katika tafiti zinazohusu usimamizi na uhifadhi ya mazingira

- Kufuatilia utekelezaji wa sera na sheria zinazohusiana na usimamizi wa mazingira

- Kufuatilia na kuanzisha maeneo yanayopaswa kuhifadhiwa

- Kupitia na kushauri kuhusu taarifa za tathmini ya athari kwa mazingira (Environmental Impact

  Assessment) na mpango mkakati wa tathmini ya mazingira (Strategic Environmental

  Assessment)

- Kuandaa na kuratibu utekelezaji wa mikakati ya matumizi salama ya teknolojia ya kisasa

   (Biosafety)

- Kufanya tathmini ya maeneo yaliyoathirika kutokana na shughuli za kiuchumi zisizoendelevu

  (kama vile uchimbaji wa madini, Kilimo, Ujenzi, Ufugaji n.k.)

- Kubainisha na kupendekeza masuala ya mazingira yanayopaswa kuhusishwa katika mipango

   ya kisekta

- Kuratibu miradi mbalimbali inayohusu usimamizi na hifadhi ya mazingira

- Kupitia taarifa ya hali ya mazingira nchini (State of the environment report) na kutoa ushauri

- Kutoa ushauri kuhusu utekelezaji wa mikataba na maazimio mbalimbali ya Kitaifa, Kikanda na

  Kimataifa kuhusu usimamizi wa mazingira

 

- Kufanya kazi nyingine zozote zinahusu usimamizi na hifadhi ya mazingira ambazo idara

   itakuwa imepangiwa.

 

Sehemu katika Idara:

Pamoja na kwamba Idara ina mtaalam mmoja, lakini Idara hii inategemea kuwa na vitengo vitatu kama ifuatavyo:

  • -Tathmini ya Mazingira, mabadiliko tabia nchi na maendeleo endelevu
  • -Udhibiti wa taka ngumu
  • -Tafiti na Elimu ya masuala mbalimbali ya mazingira
  •  

Huduma zinazotolewa na Idara:

  • -Udhibiti wa taka ngumu katika soko la Azimio, Vituo vya mabasi na maeneo ya makazi
  • -Kuratibu utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais la operesheni ya usafi kila Jumamosi ya mwisho ya mwezi.
  • - Kupitia maombi ya vibali vya ujenzi na kupitisha au kutoa ushauri pale inapohitajika
  • Kuhamasisha watu binafsi, vikundi vya kijamii na Taasisi kuandaa vitalu vya miti na kupanda miti.
  • - Kushirikisha jamii katika kuhifadhi mazingira
  • - Kutoa elimu ya hifadhi ya Mazingira na udhibiti wa taka ngumu
  • - Kufuatilia shughuli za uchimbaji wa madini usiofuata uhifadhi wa mazingira
  • - Kudhibiti uchungaji holela katika maeneo ya mjini
  • - Kufanya tathmini ya maafa na kuzitolea taarifa kwa Mwenyekiti wa kamati ya Maafa ya Wilaya

 

 

Sheria   za mazingira:  

Halmashauri ya wilaya inasimamia sheria Na. 20 ya Mwaka 2004 ya usimamizi wa Mazingira. Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imeunda sheria ndogo ya usimamizi wa Mazingira; sheria hii iliundwa Mwaka 2008.

Sheria ndogo hii ina vipengele kama ifuatavyo:

  • Uwezo wa Halmashauri katika kusimamia masuala ya mazingira
  • Wajibu wa Afisa muidhiniwa katika kusimamia sheria ndogo ya mazngira
  • Wajibu wa kila mwananchi pamoja na wamiliki wa magari kuwa na vyombo vya kukusanyia taka.
  • Ada ya ukusanyaji wa taka ngumu
  • Majukumuya wakala wa kukusanya taka ngumu
  • Viwango vya ada ya kukusanya taka katika ngazi ya kaya na kwa wadau mbalimbali

Matangazo

  • MATOKEO YA FORM FOUR 2022 - 2023 February 01, 2023
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • BILIONI 223.9 WILAYA YA TUNDURU

    March 25, 2023
  • SALAMU ZA PONGEZI

    March 19, 2023
  • MIONGOZO UENDESHAJI VYAMA VYA USHIRIKA

    March 17, 2023
  • WAKULIMA KOROSHO NA SOKO JIPYA

    March 14, 2023
  • Ona Zote

Video

MAADHIMISHO SIKU YA WANANWAKE
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.