• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Departiment
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Msingi
      • Maji
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maliasili na Utalii
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utumishi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Information, Technology, Communication and Public Relation
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Kilimo
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
      • Kata ya Mbati
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji

IDARA YA MIPANGO, TAKWIMU NA UFUATILIAJI

Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji inashughulikia upangaji na uratibu wa mipango ya maendeleo katika miaka husika, usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ya Halmashauri, Tafiti na ukusanyaji wa Takwimu pamoja na kuratibu shughuli za Uwekezaji. Idara hii ina watumishi 5 ikiongozwa na Kaimu Afisa Mipango wa Halmashauri akisaidiwa na watumishi wafuatao

Mchumi                       3

Katibu Muhtasi           1

na imegawanyika katika sehemu tano kama ifuatavyo:-

Ø Mipango na Sera

Ø Usimamizi na Ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo

Ø Tafiti na Takwimu.

 Sehemu ya Mipango na Sera

Majukumu ya sehemu hii ni kama ifuatavyo:-

Ø Kusimamia Uandaaji wa mpango wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kila mwaka.

Ø Kuratibu ufanisi wa mifuko ya Halmashauri: LGCDG, Mfuko wa Jimbo na fedha za mapato ya ndani.

Ø Uratibu na utayarishaji wa Mipango shirikishi katika Kata zote za Halmashauri kupitia Mfumo wa O&OD.

Ø Uratibu na utayarishaji wa Mpango na Bajeti ya kila mwaka ya Halmashauri.

Ø Kusimamia uandaaji wa mipango kazi (Action Plans) ya bajeti za kila mwaka na kuziwasilisha katika ngazi husika..

Ø Kuratibu uandaaji wa maandiko ya miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ø Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa sasa (BRN)

Ø Kuratibu maandalizi ya Sera na Mpango Mkakati wa Halmashauri

Ø Kuratibu uandaaji wa taarifa mbalimbali za Halmashauri pamoja na taarifa za utekelezaji wa maagizo kutoka mamlaka za juu za serikali

Ø Kuratibu na kusimamia maandalizi ya mipango ya uwekezaji ya Halmashauri.

Ø Kuratibu utekelezaji na uandaaji wa taarifa za mipango ya uwekezaji

 

Sehemu ya Usimamizi, Ufuatiliaji na Tathmini ya miradi ya

maendeleo.

Majukumu ya sehemu hii yapo kama ifuatavyo:-

Ø Kuratibu uandaaji wa taarifa za Ilani ya Uchaguzi wa CCM ya 2015 - 2020

Ø Kufuatilia utekelezaji halisi na matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo.

Ø Kuratibu miradi ya jumuiya za wananchi na taasisi nyinginezo za ndani na nje ikiwemo miradi ya wahisani

Ø Kuratibu utekelezaji wa Mipango ya muda mrefu, kati na mfupi ikiwepo Ilani ya Uchaguzi na uandaaji wa taarifa za utekelezaji wa mipango hiyo

Ø Kuratibu utekelezaji wa mipango shirikishi.

Ø Kuandaa taarifa za Miradi ya maendeleo ya Halmashauri kwa vipindi mbalimbali na kuziwasilisha kwenye mamlaka husika.

Ø Kuandaa mapitio ya bajeti ya kila mwaka baada ya kipindi cha nusu mwaka

Ø Kuandaa mapendekezo ya kubadili matumizi ya vifungu vya bajeti ya maendeleo kila inapobidi.

Ø Kuandaa taarifa za matukio ya kila wiki na kuiwasilisha ngazi ya mkoa.

Sehemu ya Utafiti na Takwimu

Sehemu hii hushughulikia masuala yanayohusu takwimu mbalimbali za kiuchumi na kijamii pamoja na kuratibu shughuli za utafiti kama ifuatavyo:-

Ø Kuratibu na kusimamia benki ya Takwimu ya Halmashauri ikihusisha takwimu za LGMD.

Ø Kuhuisha na kuboresha Takwimu za Kiuchumi na Kijamii (Profile) za Halmashauri.

Ø Kuratibu na kuhifadhi takwimu za Idadi ya watu za Halmashauri kwa kutumia rejista za wakazi wa Mitaa.

Ø Kuratibu na kutathmini utekelezaji wa Mpango mkakati wa Halmashauri 2013/14 – 2017/18

Ø Kuratibu zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.

Matangazo

  • KUITWA KAZINI TUNDURU DC July 09, 2022
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2022- 2023 January 04, 2023
  • Watumishi wa Umma walioma mwezi julai August 12, 2018
  • Orodha ya majina ya wanafunzi waliopangiwa kidato cha tano mwaka 2019 June 02, 2019
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • Pongezi kwa Dc Mtatiro

    January 26, 2023
  • Makusanyo Robo ya 1&2 Tunduru Dc Bilioni 2.5 Sawa na 54%

    January 26, 2023
  • BILIONI 26.7 ZAINGIA KWENYE MZUNGUKO KUPITIA ZAO LA KOROSHO

    January 19, 2023
  • Makabidhiano ya Gari Isuzu Tani 7 kati ya Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkurugenzi wa TAMESA

    January 18, 2023
  • Ona Zote

Video

KILO 1,147,287 ZA KOROSHO ZIMEUZWA KWENYE MNADA WA SABA TUNDURU DC
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Taarifa ya Ukimwi kuishia decemba 2017
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.