WILAYA YA TUNDURU YAPATIWA DAWA ZA KUKINGA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE
Wilaya ya Tunduru imepokea dawa za kukinga Magonjwa mbalimbali yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (NTDs), ambapo zoezi la Ugawaji Ngazi ya jamii linatarajiwa kuanza February 23, 2024.
Hayo yamesemwa na Mratibu wa zoezi la ugawaji dawa hizo za kinga, Ndg. Baraka Mmari, katika mafunzo ya jinsi ya ugawaji dawa katika ngazi ya jamii, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Hospitali ya Wilaya ya Tunduru.
Alisema, Zaidi ya watu 400,000 watapatiwa dawa kinga dhidi ya magonjwa haya katika vijiji vyote 157 vilivyopo katika Wilaya ya Tunduru, ambapo zaidi ya Milioni 200 zitatumika kukamilisha zoezi hilo.
Ndg. Mmari aliwataka watoa huduma ya ugawaji dawa kwenda kutoa elimu Kwa jamii kuhusu namna bora ya kujikinga na Magonjwa haya. Alisema kuwa elimu ni muhimu sana kwa sababu itasaidia jamii kuelewa umuhimu wa kutumia dawa za kinga na jinsi ya kuzitumia kwa usahihi.
Aidha, Aliwasisitiza watoa huduma hao, kuhakikisha wanatembelea kila kaya na kutoa Huduma hiyo, pia kuhakikisha kila Mwananchi anapatiwa huduma hiyo ya dawa kinga za Magonjwa hayo.
“Tunaamini bila ninyi zoezi hili haliwezi kukamilika, tunaomba tuoneshe uzalendo katika kufanya hili zoezi ili tuzidi kuimalisha afya katika Wilaya yetu”. Alisema Mmari.
Mmari alitoa taaria ya Baadhi ya magonjwa yaliokuwa hayapewi kipaumbele yanayoathiri Wilaya hii ni pamoja na usubi, Kichocho, ugonjwa wa minyoo, ugonjwa wa Matende na Mabusha
Aidha, Bw. Mmari alitoa wito kwa Wananchi kuonesha ushirikiano kwa watoa huduma hao pale tu wanapofika katika makazi yao, kwani zoezi hili linakwenda kuimarisha afya zetu katika jamii.
Mafunzo haya yalihudhuriwa na watoa huduma ya ugawaji dawa hizo kutoka katika ngazi ya Jamii kutoka katika Vitongoji vyote vilivyopo Wilaya ya Tunduru . Ambapo Watoa huduma hawa watawajibika kwa ugawaji wa dawa za kinga kwa jamii katika Vitongoji vyao katika kila kaya.
Baadhi ya Watoa huduma za kugawa Dawa kinga wakitoa maoni kuhusu Magonjwa yaliyokuwa hayakupewa kipaumbele.
Mratibu wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.