• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

TUNDURU Yajizatiti Kukabiliana na Ugonjwa wa Mpox.

Imewekwa : March 27th, 2025

Leo, tarehe 27 Machi 2025, kikao muhimu cha huduma za afya ya msingi kilifanyika wilayani Tunduru. Lengo kuu la kikao hicho lilikuwa kujadili na kuweka mikakati ya tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Mpox. Kikao hicho kiliwakutanisha viongozi wa serikali, wataalamu wa afya, na wadau mbalimbali kutoka ndani ya wilaya.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Tunduru, Ndugu Milongo Sanga, alimwakilisha mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mheshimiwa Simon Chacha, alitoa wito kwa wananchi kutozua taharuki. Alisisitiza kuwa hadi sasa, hakuna mgonjwa wa Mpox aliyeripotiwa wilayani humo. Alihimiza uzingatiaji wa masharti na maelekezo ya wataalamu wa afya ili kujikinga na ugonjwa huo.

Pichani ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Tunduru, Ndugu Milongo Sanga

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru, Grace A. Mhagama, alisisitiza kuwa wote waliohudhuria kikao hicho wawe mabarozi wazuri ili kila mmoja achukue tahadhari juu ya ugonjwa huu. Aliongeza kwa kuzungumza kwamba kila mwananchi ana jukumu la kuelimisha wengine kuhusu dalili, njia za maambukizi na namna ya kujikinga na ya ugonjwa wa Mpox.

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi, Daktari Athumani Mkonoumo, katika mada yake, alielezea dalili za ugonjwa huo, namna unavyoambukizwa na jinsi ya kujikinga, na pia alibainisha kuwa Mpox ni ugonjwa ambao hadi sasa hauna dawa ya moja kwa moja. Alifafanua kuwa wagonjwa wanaopatikana na ugonjwa huo hupewa matibabu kulingana na dalili wanazozionesha, huku wakitengwa na watu wengine ili kuzuia maambukizi.

Pichani ni Mganga Mfawidhi wa wilaya ya Tunduru, Daktari Athumani Mkonoumo

Afisa Afya wa Wilaya Bwana. Ayubu Majumbewima alieleza kuhusu hali ya utayari wa kukabiliana na ugonjwa wa Mpox tangu Wizara ya Afya ilipotoa tangazo la uwepo wa ugonjwa huu nchini. Alisema Halmashauri ya Wilaya imechukua hatua mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa jamii kupitia kliniki za akina mama, siku za lishe, mashuleni, mikutano ya hadhara, na vijiwe. Pia, mabango yenye taarifa kuhusu ugonjwa huo yamesambazwa na kubandikwa, na elimu inatolewa kupitia redio.

Pichani ni Afisa Afya wa Wilaya Bwana. Ayubu Majumbewima.

Aidha, Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imetenga jengo maalum kwa ajili ya kuwatenga wagonjwa watakaobainika kuwa na dalili za Mpox. Pia, gari limetayarishwa kwa ajili ya usafiri wa wataalamu wa afya na wagonjwa.

Viongozi wa afya walisisitiza ushirikiano kutoka kwa jamii ili kuhakikisha ufanisi katika kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo. Ushirikiano huu unajumuisha kutoa taarifa sahihi, kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya, na kuepuka tabia zinazoweza kuhatarisha afya.

Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • SULUHU YA KUDUMU Maji Tunduru Yapatikana: Mkataba Wa Bilioni 3.2 Wasainiwa

    May 07, 2025
  • BODI Ya Wakurugenzi wa Mamlaka Ya Maji Na Usafi Wa Mazingira Tunduru (TUUWASA) Yazinduliwa

    May 07, 2025
  • TUNDURU Yajizatiti Kukabiliana na Ugonjwa wa Mpox.

    March 27, 2025
  • TUNDURU Yaungana katika Dua na Iftar

    March 24, 2025
  • Ona Zote

Video

WANANCHI WAENDELEA KUPATIWA MAFUNZO KWA VITENDO ILI KUTATUA MIGONGANO YA BINADAMU NA WANYAPORI.
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.