Katibu Tarafa wa Tarafa ya Nakapanya, Bi. Asia Lugome, amefanya uzinduzi wa upandaji Miti katika Tarafa hiyo katika Kata ya Ngapa Februari 20, 2024.
Hafla ya uzinduzi ilifanyika katika Shule ya Msingi Ngapa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waheshimiwa Madiwani, Watendaji wa Kata na Vijiji, Wenyeviti wa Vijiji pamoja na wananchi.
Katika tukio hilo, Bi. Lugome aliongoza zoezi la upandaji miti ambapo jumla ya miche 500 ya miti mbalimbali ikiwemo ya vivuli ilipandwa.
Akizungumza baada ya tukio hilo, Bi. Lugome amewapongeza viongozi na wananchi wa Tarafa ya Nakapanya kwa kushiriki kikamilifu katika zoezi la upandaji Miti. Alihimiza kila mtu kushiriki katika utunzaji wa Mazingira kwa kupanda miti na kuepuka ukataji miti ovyo.
"Utunzaji wa mazingira ni jukumu la kila mwananchi," alisisitiza Bi. Lugome. "Tupande miti, tusikate miti hovyo kuendana na mabadiliko ya tabia nchi."
Zoezi la upandaji Miti katika Tarafa ya Nakapanya ni sehemu ya kampeni ya Wilaya ya upandaji Miti.
Ambapo Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Wakili. Julius S. Mtatiro aliagiza kuwa kampeni hii iendelee katika kila Tarafa na kila kata, ambapo Kampeni hii inalenga kupanda Miti zaidi ya 200,000 ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
"Tuna wajibu wa kuitunza dunia yetu kwa ajili ya vizazi vijavyo," alisema Mhe Mtatiro. "Tuwe mfano bora kwa kuonyesha upendo kwa mazingira.".
Mbali na upandaji Miti, Bi. Lugome pia alitoa wito kwa wananchi kutunza Mazingira kwa kuepuka uchafuzi wa Mazingira na kuhifadhi vyanzo vya maji.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.