• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

Shida ya Maji Amani sasa Basi.

Imewekwa : March 23rd, 2018


 

Katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji duniani Halmashauri ya wilaya ya Tunduru iliyopo katika mkoa wa Ruvuma   wameungana na nchi nyingine zote duniani kufanya sikukuu hiyo katika Kijiji cha Amani ambapo mradi mkubwa wa maji wa Amni umekabidhiwa kwa wananchi wa vijiji vya Amani,Chiungo,Meamtwaro na Mchengamoto.

Akisoma risala ya utekelezaji wa mradi wa maji Amani kwa mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya Tunduru Ndg Eberhard Halla unaodhaminiwa na benki ya dunia alisema kuwa mradi wa maji Amani umegharimu jumla shilingi milioni 978,445,572.50. hadi kukamilika.

Alisema mradi huu wa maji Amani jumla ya vituo vya kutolea huduma ya maji 48 vimejengwa katika vijiji vya Amani 17, Chiungo 10, Meamtwaro 8, Mchengamoto 10 na kitongoji cha Mkarachani 3 ambapo mradi huu unatumia chanzo kimoja cha maji cha mto Nambango kilichpo Kijiji cha Amani.

Kaimu Afisa Utumishi wilaya Ndg John Mpangala akifanya utambusho wa viongozi katika maadhisho ya kilele cha wiki ya maji Duniani ambayo kiwilaya yamefanyika katika Tarafa ya Namasakata.

Akihutubia wananchi wa kata ya Namasakata katika kilele cha wiki ya maji duniani mgeni  rasmi ambaye pia ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Tunduru Mh Mbwana Mkwanda Sudi alisema kwanza mradi anaoukabidhi kwa wananchi wa vijiji vinne vya Chiungo, Amani, Mchengamoto na Meamtwaro ni miongni mwa miradi 10 katika vijiji kumi vya Tunduru inayofadhiliwa na benki ya dunia.

Mh.Mkwanda Sudi aliendelea kusema kuwa katika maadhimisho ya wiki ya maji duniani inayoanza tarehe 16 hadi kilele chake tarehe 22 machi kila mwaka shughuli zifuatazo hufanyika kutoa elimu ya uhamasishaji juu sera za maji nchini, elimu ya utunzaji wa mazingira na namna ya kutunza na kulinda vyanzo vya maji.

Aidha mwenyekiti aliwataka wananchi kuchangia mradi huo ili uwe endelevu na udumu kwani serikali imewekeza fedha nyingi sana katika mradi huu na maeneo mengi ya Wilaya ya Tunduru wanatamani kupata mradi kama huo, hivyo niwatake madiwani wa Kata ya Namasakata na Misechela ambao wanapata huduma ya maji kuhamasisha wananchi juu ya umuhimu wa kutunza, kuchangia na kulinda mradi huu.

Kaimu mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Tunduru ndg Eberhad Halla akikabidhi Taarifa ya utekelezaji wa mradi wa maji Amani uliogharimu Jumla ya shilingi milioni 978,445,572.50. hadi kukamilika, mradi huu umewafikia wananchi wa vijiji vinne vya Amani, Mchangamoto, Chiungo, Meamtwaro pamoja na kitongoji cha Mkarachani

Mwenyekiti alisema “ni nyema vijiji vikajiwekea utaratibu wa kuchangia huduma ya maji ili mradi uwe endelevu lakini kuna makundi maalum katika jamii ambayo sio lazima kuchangia mfano wazee na walemavu hawa inabidi kukadiriwa kiwango cha lita za maji wanazotumia kwa siku”

Vilevile aliwakumbusha wananchi juu ya suala zima la utunzaji wa mazingira na kulinda chanzo cha maji cha mto Nambango, ni vyema kujikinga na magonjwa mtambuka ambayo hayana tiba kama ukimwi na magonjwa yanayosababishwa na uchafu wa mazingira kama kipindupindu na malaria.

Wanakijiji wa kijiji cha Amani wakiwa katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya maji Duniani kilichofanyika katika Tarafa ya Namasakata wilayani Tunduru.

Alihitimisha kwa kutilia mkazo katika sula zima la wananchi kuthamini elimu kwani ndio urithi pekee watakaowaachia watoto wao, hivyo niwaagize wanafunzi wazazi na walezi kuacha tabia za kuwazua watoto wao kwenda shule na pia kuacha tabia za kuwahamasisha kufanya vibaya katika mitihani ya darasa la saba kwani elimu inatolewa bure, na azma ya serikali ni kuona kuwa watoto wote wanapata elimu bora.


Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • SULUHU YA KUDUMU Maji Tunduru Yapatikana: Mkataba Wa Bilioni 3.2 Wasainiwa

    May 07, 2025
  • BODI Ya Wakurugenzi wa Mamlaka Ya Maji Na Usafi Wa Mazingira Tunduru (TUUWASA) Yazinduliwa

    May 07, 2025
  • TUNDURU Yajizatiti Kukabiliana na Ugonjwa wa Mpox.

    March 27, 2025
  • TUNDURU Yaungana katika Dua na Iftar

    March 24, 2025
  • Ona Zote

Video

WANANCHI WAENDELEA KUPATIWA MAFUNZO KWA VITENDO ILI KUTATUA MIGONGANO YA BINADAMU NA WANYAPORI.
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.