Hayo yamesemwa na waratibu elimu Kata baada ya kukabidhiwa Pikipiki na mwakailishi wa katibu mkuu TAMISEMI Ndg Salum Mohamed Mkuya kwa ajili ya kufanya usimamizi na ufuatiliaji wa masuala ya Elimu wilayani Tunduru mapema wiki hii.
Akitoa shukrani kwa rais Dk John Pombe Magufuli kwa kuboresha mazingira ya kazi ya walimu na mazingira ya kufundishia mratibu Elimu Kata Tuwemacho ndg Fulko Makota alisema “tulikuwa tukipata changamoto sana ya namna ya kufanya kazi kutokana na jeografia ya shule tunazosimamia kuwa na umbali kutoka shule moja kwenda nyingine, hivyo kwa pikipiki hizi kazi zetu za usimamizi na ufuatiliaji zitakuwa rahisi na kufanyaika kwa ubora uliokubalika”
Vilevile tunahidi kwako mkuu wa wilaya pamoja mawaziri wa wizara za sayansi na teknolojia na ofisi ya rais Tamisemi kuwa tunalenga katika kuinua kiwango cha ufaulu wilayani Tunduru na kutoa huduma bora kwa shule tunazosimamia.
Na kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mh.Juma Zuberi Homera aliwataka waratibu elimu kata kutumia pikpiki hizo kwa kazi ya usimamizi , ufuatiliaji wa elimu ili kuhakikisha kuwa wanainua kiwango cha ufaulu wilayani Tunduru kwa mwaka 2018.
Aidha Juma Homera amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kuendelea kutekeleza sera ya elimumsingi bure, kuboresha Miundombinu ya Shule na kuendelea kuajiri watumishi wa idara mbalimbali hasa Afya na Elimu.
Alisema “halmashauri ya wilaya ya Tunduru ina upungufu mkubwa wa Walimu hasa wa masomo ya sayansi kwa shule za sekondari na baadhi ya shule za msingi kuwa na walimu wawili na mmoja kwa baadhi ya shuel hali ambayo inasababisha watoto wetu kutopata elimu bora”
Mkuu wa wilaya ya Tunduru alimuomba Bwana Salum Mkuya aliyemuwakilisha katibu mkuu Tamisemi kukabidhi Pikipiki kwa waratibu elimu kata Kufikisha kilio cha wanatunduru kwa Katibu Mkuu Tamisemi cha Upungufu wa watumishi katika sekta ya elimu ili kuwasaidia watoto wa wakulima wanaokosa elimu bora kutokana na uchache huo.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.