Wananchi wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma watekeleza agizo la mkuu wa Wilaya Ndg Juma Homera lililotolewa mwaka 2016 agosti la kila kaya kulima jumla ya Ekari tano za mazao mchanganyiko na kila kata Ekari 10 ili kuboresha maisha ya wananchi na kuongeza kipato cha familia.
Hayo yamesemwa na wananchi wa wilaya ya Tunduru wakati wa ziara ya ukaguzi wa mashamba iliyofanywa na mkuu wa wilaya ya Tunduri Ndg Juma Homera ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya kila mwananchi kulima shamba la Ekari tano za mazao mchanganyiko.
“Nawashukuru wananchi wa wilaya ya Tunduru kwa mwitikio mkubwa wa kushiriki katika kilimo cha mazao mchanganyiko katika maeneo mbali mbali ya wilaya kwa kulima mazao kama mahindi, mbaazi,mihogo,kunde”
Wakitoa ushuhuda kwa mkuu wa wilaya uongozi wa Kata ya Nandembo wakishikiana na Afisa Kilimo wa Kata namna alivyoweza kutekeleza agizo hilo lililotolewa na mkuu wa wilaya mwaka Jana mwezi Agosti alisema
“Tulipokea maagizo ya mkuu wa wilaya na kuanza kuyafanyia kazi kwa kuwahimiza wananchi kwa kila kaya kuandaa mashamba msimu wa kilimo na walikuwa na mwitikio mkubwa sana na katika kata ya Nandembo tumelima jumla ya Ekari 13 na robo za mazao mchanganyiko kama Mahindi,Mbaazi na Mihogo”
Sambamba na utekelezaji wa magizo ya serikali wananchi wa kata ya nandembo wamekumbana na changamoto mbali mbali ikiwemo uchache wa wataalamu wa kilimo,uchache wa pembejeo za kilimo, mabadiliko ya Tabia ya nchi, ucheweleshaji wa malipo ya korosho hali iliyochangia wananchi kushindwa kununua pembejeo kwa wakati.
Aidha mkulima wa kijiji cha Legezamwendo Ndg Matumila Waziri amefanikiwa kulima ekari tano za mahindi ,karanga, nyanya na mpunga na anasema kupitia agizo la mkuu wa wilaya sasa anaweza kupata chakula cha kutosha,kupata fedha ya kuwasomesha watoto wake atakapovuna kwani mwaka huu atapata mavuno mengi kulinganisha na miaka ya nyuma.
"Nimevuka lengo na nimelima ekari sita na matarajio yangu ni kuvuna vizuri,na nitasomesha,na chakula kitakua cha kutosha hivyo hakuna njaa kabisa"
Hata hivyo ziara ya ukaguzi iliendelea hadi Kijiji cha Naluwale Kata ya Nandembo na kujionea shamba la mfano la bibi Salome Kalemwa ambaye amefanikiwa kulima ekari tatu za mahindi na mbaazi na kuonesha na kushukuru mchango wa Afisa kilimo wa Kata na uhamasishaji unaofanywa na uongozi wa Kata katika kuhakikisha wananchi wanashiriki katika kilimo.
Bi Salome alisema kuwa anaiomba serikali kusimamia malipo ya korosho yafanyike kwa wakati ili kuwawezesha wakulima kununua pembejeo kwa wakati kutokana na mwaka huu kuathiriwa kwa kiasi kikubwa kutokana na ucheleweshaji wa malipo.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.