• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

MKURUGENZI MTENDAJI WILAYA AFANYA UZINDUZI WA MAFUNZO YA TUSOME PAMOJA.

Imewekwa : October 5th, 2017

Mafunzo ya tusome pamoja ni mradi unaotekelezwa na Shirika la  Maendeleo  la Kimataifa la  Watu wa Marekani (USAID) unaolenga kusaidia kuboresha stadi za za kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) katika shule za awali na madarasa ya chini ya shule za msing (1-4) katika mikoa minne ya Tanzania bara (Ruvuma, Mororgoro,Mtwara,Iringa) pamoja na shule zote za serikali zanzibar.

USAID Tusome pamoja kwa kushirikiana na serikali walitoa mafunzo  mkoa wa Ruvuma ya mpango Jamii wa uhamasishaji na utekelezaji Elimu (MJUUE) wenye lengo la kuhamasisha jamii katika kubaini changamoto katika sekta ya elimu  msingi zinazoathiri ubora wa elimu na ufaulu. Pia kuisaidia jamii ishiriki katika kuandaa mipango ya elimu kwa ajili ya watoto wao hivyo kuimarisha ushiriki wa jamii katika kuboresha utoaji elimu.

Mratibu wa mafunzo hayo ya USAID Tusome pamoja alisema kuwa walitoa mafunzo ya siku tatu ya wawezeshaji jamii Elimu 1,400 kutoka shule 770 za msingi za serikali mkoani Ruvuma ambao pamoja namambo mengine wameweza kusaidia kuongoza uaandaaji wa wa dira na mipango kazi ya muda mfupi ya shule za msingi na mipango hiyo kuridhiwa na jamii, wahamasishaji watafanya kazi kwa kujitolea kuhamasisha jamii kushiriki katika shughuli zote zinazohusu elimu katika shule zao.

vile vile leo tarehe 05/10/2017 ni muendelezo wa mafunzo waliyopata awali na watatoa mrejesho wa shughuli walizofanya katika maeneo yao katika kuandaa mipango kazi ya muda mfupi ya shule za msingi na mipango hiyo kuridhiwa na jamii.

Akizungumza na wahamasishaji kutoka katika kata za wilaya ya tunduru kaimu mkurugenzi mtendaji (W) mwalimu George Mbesigwe ambaye ni Afisa Elimu Vifaa na Takwimu aliyemuwakilisha mkurugenzi mtandaji alisema mafunzo haya yamefanyika kwa awamu ya pili na yale ya awamu ya kwanza yalienda vizuri kwani wameandaa mpango lakini utekelezaji umeanza kufanyika kwani kuna baadhi ya shule ambazo zimeanza tayari kujenga matundu ya choo.

"nimepita katika shule ya msingi mjimwema nimekuta wanafyatua Tofali kwa ajili ya kuongeza matundu ya vyoo ni namna gani mafunzo haya yana mrejesho chanya kwa jamii na kuleta mabadiliko"

Alisema pamoja na serikali na wadau wa maendeleo kuwezesha mradi wa uaandaji wa mipango lakini kumbukeni kuwa shule ni mali ya jamii na huo ni wajibu wa kila mtu kujua hilo na tunapotekeleza miradi yetu katika maeneo yetu tujue kuwa tunafanya kwa ajili yetu na sio kwa ajili ya serikali.

pia niwakumbushe lengo la mradi wa tusome pamoja unaofadhiliwa na shirika la maendelo la kimataifa la watu wa marekani kuleta hamasa kuanzia ngazi ya chini kabisa ya familia mpaka ngazi ya juu ili wanafunzi wetu wote wapate elimu bora pamoja na kuwasilisha mipango yenu lakini pia ni vizuri kuwasilisha na changamoto mlizokumbana nazo katika kuandaa mpango huu.

lakini najua kuna uwakilishi wa watu wawili tu ni matumaini yangu kuwa yale mtakayojifunza hapa mtaenda kuwashirikisha jamii yote kwa ujumla ili kuweza kuyatekeleza kwa manufaa ya jamii yetu na kufikia malengo tuliyojipangia.

Hata hivyo mipango inawasilishwa katika halmashauri ya wilaya ya Tunduru na mipango waliyopanga ni yale mambo watakayofanya kutekeleza mipango yao na baadhi ya mipango yao itajumuishwa kwenye mpango wa serikali ya mwaka wa fedha ujao.

Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • SULUHU YA KUDUMU Maji Tunduru Yapatikana: Mkataba Wa Bilioni 3.2 Wasainiwa

    May 07, 2025
  • BODI Ya Wakurugenzi wa Mamlaka Ya Maji Na Usafi Wa Mazingira Tunduru (TUUWASA) Yazinduliwa

    May 07, 2025
  • TUNDURU Yajizatiti Kukabiliana na Ugonjwa wa Mpox.

    March 27, 2025
  • TUNDURU Yaungana katika Dua na Iftar

    March 24, 2025
  • Ona Zote

Video

WANANCHI WAENDELEA KUPATIWA MAFUNZO KWA VITENDO ILI KUTATUA MIGONGANO YA BINADAMU NA WANYAPORI.
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.