• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

Michezo ni afya na ni ajira

Imewekwa : May 12th, 2019

Na Theresia Mallya -Tunduru

Katika utekelezaji wa sera ya michezo ya  serikali ya awamu ya tano ya kuhamasisha kusimamia michezo katika ngazi zote hapa nchini kwa kuendeleza matamasha ya michezo kuanzia ngazi za vijiji,kata, wilaya, mkoa hadi taifa, uzinduzi wa ligi ya DC Homera Cup  imezinduliwa na mkuu wa wilaya ya Tunduru Mhe.Juma Zuberi Homera mwishoni mwa juma.

Akizungumza katika uzinduzi wa ligi ya DC Homera Cup uliofanyika katika viwanja vya kijiji cha Nangunguru Kata ya Nandembo mkuu wa wilaya ya Tunduru Mhe.Juma Zuberi Homera alisema mashindano haya ni kwa ajili ya kupata timu 16 zitakazowakilisha tarafa katika michezo ngazi ya wilaya.

wachezaji wa timu ya super wakiwa katika maandalizi ya ufunguzi wa mechi kati yao na timu ya chimbuko kutoka katika kijiji cha majala katika Mechi ya ufunguzi wa ligi ya DC Homera Cup inayotimua vumbi katika viwanja mbalimbali wilayani Tunduru.

“Mashindano haya yanalenga kupata timu mbili kutoka kila tarafa zitakazowakilisha tarafa kwenye  mashindano  ngazi ya wilaya na baadaye kupata timu moja ya wilaya” alisema mkuu wa wilaya ya Tunduru.

Mkuu wa wilaya aliahidi zawadi zifuatazo kutolewa kwa washindi ngazi ya tarafa ikiwa ni pamoja na mshindi wa kwanza kupewa zawadi ya jezi,mpira na  fedha tsh 150,000, mshindi wa pili  fedha taslimu laki moja, jezi, na mpira ana mshindi wa tatu kupata jezi na fedha shilingi sitini elfu (50,000).

Akitaja zawadi nyingine zitatolewa kwa timu yenye nidhamu, mfungaji bora na  mwamuzi aliyechezasha mechi kwa kuzingatia kanuni 17 za fifa.

Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mhe.Juma Zuberi Homera akifuatilia mechi ya Ufunguzi wa Ligi ya DC Homera Cup iliyopigwa na timu ya chimbuko kutoka kijiji cha majala na super ego ya kijiji cha Nangunguru iliyopigwa katika kiwanja cha Kijiji cha Nangunguru ambapo hadi mchezo unaisha walitoshana nguvu ya Goli 1-1.

Kwa upande wa wachezaji na walimu wao walipongeza kuanzishwa kwa ligi ya DC Homera Cup kwani inaongeza hamasa kwa wananchi na kutoa fursa kwa vijana kuonesha vipaji vyao, kujenga umoja na ushirikiano kati ya kijiji na kijiji, kata na hata tarafa, na kufahamiana,zaidi fursa ya kusongambele zaidi katika kufikia ndoto walizojiwekea.

“Tunaomba michezo hii iwe endelevu angalau ifanyike mara mbili au tau kwa mwaka kwa ajili ya kuwajenga vijana wetu, na wadau wengine wajitokeze katika kusapoti michezo katika wilaya yetu” alisema mwalimu wa timu ya Chimbuko ya kijiji cha Majala.

Naye mwalimu wa timu ya Sevenup kutoka Kata ya Namakambale Bw. Mkakia aliomba usimamizi wa chama cha michezo wilaya kuwa wabunifu ili kuendeleza michezo ndani ya wilaya na kuwaunganisha wakazi wa Tunduru kwani wapo vijana wengi wenye vipaji lakini hawapati nafasi ya kujiendeleza.

Tunampongeza sana Mkuu wetu wa Wilaya kuanzisha ligi hii kwani inatoa hamasa kwa vijana wengi na wananchi wanapenda michezo sana, niwaombe vingozi wa chama cha michezo wilayani Tunduru muendeleze michezo na kuwa wabunifu ili tutengeneze timu zitakazotufikisha mbali zaidi ya hapa tulipo sasa” alisema Mkaki mwalimu wa timu ya Sevenup Namakambale.

Hata hivyo ligi hii ya DC Homera Cup inatimua vumbi katika viwanja mbalimbali katika tarafa zote saba (7) za  Mlingoti, Nampungu, Matemanga, Nakapanya, Namasakata, Nalasi na Lukumbule kwa lengo la kuhamasisha lakini pia kuibua vipaji kwa vijana wengi na kutoa fursa ya ajira.

Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • SULUHU YA KUDUMU Maji Tunduru Yapatikana: Mkataba Wa Bilioni 3.2 Wasainiwa

    May 07, 2025
  • BODI Ya Wakurugenzi wa Mamlaka Ya Maji Na Usafi Wa Mazingira Tunduru (TUUWASA) Yazinduliwa

    May 07, 2025
  • TUNDURU Yajizatiti Kukabiliana na Ugonjwa wa Mpox.

    March 27, 2025
  • TUNDURU Yaungana katika Dua na Iftar

    March 24, 2025
  • Ona Zote

Video

WANANCHI WAENDELEA KUPATIWA MAFUNZO KWA VITENDO ILI KUTATUA MIGONGANO YA BINADAMU NA WANYAPORI.
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.