UTEKELEZAJI WA MFUMO WA USAFIRISHAJI WA DHARURA WAJAWAZITO NA WATOTO WACHANGA.
"Kila mwaka katika nchi yetu akina mama wapatao 2,370,000 wanajifungua, kati yao elfu 45 wanapata dharura ya kuhitaji usafiri kwenda kwenye vituo vinavyotoa huduma stahiki za afya ,ili wapate kusaidiwa, serikali kupitia wanaushirika wa maendeleo waliweza kuzindua mpango wa usafirishaji wa dharura wa akina mama wajawazito na watoto wachanga (M-mama) ili kuhakikisha wanawake hawa na watoto wao wanapata usafiri wanapokuwa katika hali ya dharura ili kufanya maisha yao yasiwe hatarini" (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania).
Katika utekelezaji wa mfumo wa usafirishaji wa dharura wajawazito na watoto wachanga ,leo yamefanyika mafunzo elekezi kwa madereva na wenye magari binafsi kwenye jamii katika halmashauri ya wilaya ya Tunduru, ambapo katika mafunzo hayo walipata kufahamu mfumo huo wa rufaa na usafirishaji wa dharura ,usafi na usalama wakati wanatimiza jukumu hilo na pia mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kufanya usafirishaji wa dharura, mafunzo hayo yaliwezeshwa na Victor Romward programm officer Pathfinder internetinal , sifaely waynse ,program officer Pathfunder internatinal (Ruvuma) na Frida Metha ,Mratibu M-mama mkoa.
Aidha maratibu wa M-mama wilaya ya tunduru Ndg. Renatus mathias alisema , sisi leo tumefanya mafunzo kwa madereva watakaoshiriki katika kusafirisha wajawazito na watoto wachanga kuwapeleka katika vituo stahiki kwaajili ya huduma za haraka, alisema maradi huu rasmi utaanza kufanya kazi katika wilaya ya Tunduru kuanzia mwezi agosti mwaka huu ,alisema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwapatia elimu juu ya kuhudumia wakati wa majuku hayo ya kusafirisha wajawazito na watoto wachanga , na lengo kuu la mradi huu ni kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi hasa kwa kucheleweshwa kwa wakina mama wajawazito na watoto wachanga kwenye kwenye vituo vya kitolea huduma za afya.
Kwa niaba ya jamii , mzee Mohamedi Gwaya kutoka kata ya mbesa ameipongeza serikali na wadau wa maendeleo kwa ujumla waliowezesha mradi huu wa M-mama kwa kuwa unakuja kuwa mkombozi kwa jamii hasa za vijijini kwa kuwezesha sasa uwezekano wa haraka wa kuwafikisha akina mama wajawazito na watoto wachanga katika vituo vya afya kwa haraka na urahisi.
Mafunzo hayo yalihitimishwa kwa ujazwaji wa mikataba ya makubaliano kwa madereva jamii kushiriki kikamilivu katika mradi huu wa usafirishaji wa dharura wajawazito na watoto wachanga (M-mama) katika wilaya ya Tunduru.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.