• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

MADIWANI WANAWAKE WAWAFUNDA NANDEMBO SEKONDARI

Imewekwa : February 9th, 2024

MADIWANI WANAWAKE WAWAFUNDA NANDEMBO SEKONDARI.

Umoja wa Waheshimiwa Madiwani Wanawake wilaya ya Tunduru, ukishirikiana na idara ya Maendeleo ya jamii, ustawi wa jamii Pamoja  na Dawati la Jinsia na watoto, wamefanya ziara katika shule ya Sekondari Nandembo Februari 08, 2024.

Lengo kuu likiwa kuzungumza na watoto wa Kike masuala mbalimbali yawahusuyo, hasa katika umri waliopo , ambapo mada mbali mbali zilizungumzwa na Wataalamu na Waheshimiwa Madiwani kwa ujumla.

Wakizungumza na Wanafunzi  hao , Waheshimiwa Madiwani waliwahimiza  Wanafunzi kuzingatia sana Elimu  na kuwa na nidhamu, na maadili mema   wakati wote katika jamii inayowazunguka, waliwataka Wananfunzi hao kutojihusisha na Mahusiano ya kimapenzi kwani kufanya hivyo kutapelekea kuaharibu malengo yao ya baadae,Sambamba na ilo waliwataka kujiepesha zaidi na Mimba za utotoni

Kwa upande wao wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, walitoa Elimu kuhusu aina mbalimbali za ukatili, jinsi ya kujikinga na ukatili, na wapi pa kupata msaada iwapo watapata athari za ukatili,

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa wanawake Wilaya ya Tunduru, Bi. Fatu Jabari, alisema kuwa lengo la ziara hiyo ni kuwafikia vijana hasa Wanafunzi wasichana  na kuwaelimisha kuhusu ukatili ili waweze kujikinga na pia kupambana na tatizo hili katika jamii.

"Tunajua kuwa ukatili ni tatizo kubwa linaloathiri wanawake na watoto wengi nchini Tanzania," alisema Bi. Jabari. "Kwa hiyo, ni muhimu kuwapa vijana maarifa na ujuzi wa kujikinga na ukatili na pia kupambana na tatizo hili."

Wanafunzi walifurahishwa sana na elimu waliyoipata na waliwashukuru madiwani hao kwa kuwajali na kuwapa maarifa muhimu. Waliahidi kuwa watatumia elimu hiyo kujikinga na ukatili na pia kuwaelimisha wenzao na jamii kwa ujumla.

Diwani wa Kata ya Nandembo Mhe. Omari Malipesa, aliwashukuru waheshimiwa Madiwani wanawake hao kwa kutembelea shule hiyo na kuwapa wanafunzi elimu muhimu.

"Elimu hii ni muhimu sana kwa wanafunzi wetu," alisema Diwani Malipesa. "Itawasidia kujikinga na ukatili na pia kuwawezesha kuwa na maisha bora ya baadaye."

Ziara hii ni sehemu ya kampeni ya Umoja wa wanawake Wilaya ya Tunduru ya kupambana na ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto. Kampeni hii inalenga kuwafikia wananchi wa Wilaya ya Tunduru na kuwaelimisha kuhusu ukatili na jinsi ya kupambana na tatizo hili.

Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • SULUHU YA KUDUMU Maji Tunduru Yapatikana: Mkataba Wa Bilioni 3.2 Wasainiwa

    May 07, 2025
  • BODI Ya Wakurugenzi wa Mamlaka Ya Maji Na Usafi Wa Mazingira Tunduru (TUUWASA) Yazinduliwa

    May 07, 2025
  • TUNDURU Yajizatiti Kukabiliana na Ugonjwa wa Mpox.

    March 27, 2025
  • TUNDURU Yaungana katika Dua na Iftar

    March 24, 2025
  • Ona Zote

Video

WANANCHI WAENDELEA KUPATIWA MAFUNZO KWA VITENDO ILI KUTATUA MIGONGANO YA BINADAMU NA WANYAPORI.
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.