• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Departiment
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Msingi
      • Maji
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maliasili na Utalii
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utumishi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Information, Technology, Communication and Public Relation
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Kilimo
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
      • Kata ya Mbati
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI ROBO YA PILI

Imewekwa : May 2nd, 2022

Madiwani wa Halmashsuri ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma wameipongeza Serikali Kwa kuipatia fedha Nyingi zilizo iwezesha Halmashauri yao kutekeleza Miradi mingi

Hayo yalibainishwa katika kikao cha cha baraza la madiwani cha Robo ya pili ya mwaka 2022 kilicho fanyika katika ukumbi wa Klasta ya Walimu wa Baraza la Mlingozi mjini hapa na kwamba katika kipindi cha mwaka mmoja jumla ya shilingi Bilioni 2.110 zimeletwa na serikali.

Alisema katika kipindi hicho halmashauri ilipokea kiasi cha shilingi Bilioni1.410 kwa ajili ya Ujenzi wa shule tatu mpya za sekondari katika Kata za nakayaya, Lukumbule na majimaji.

Alisema sambamba na fedha hizo pia katika kipindi hicho jumla ya shilingi milioni 700 zilizo tumika kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya vituo vya afya 2 na zahanati 4 zikiwa ni juhudi za serikali kusogeza huduma kwa jamii.

Aidha Mh.Hairu Hemedi Mussa  pia akatumia nafasi hiyo kuwapongeza viongozi wa Halmashauri hiyo kwa ushirikiano walioufanya kipindi cha mapokezi ya mwenge wa uhuru zilizofanyika April 15-16/ mwaka huu ambapo hakuna mradi ulio kataliwa.

Kwa upande wake Katibu wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Tunduru Mwl. Mohammed Mavala pamoja na mambo mengine alisema kuwa pamoja kutokuwepo kwa miradi ya mwenge iliyokataliwa lakini zipo dosari ambazo zimekuwa zikijitokeza katika ujenzi wa miradi ya serikali.

Aidha katika taarifa Mavala akamtaka mwenyekiti wa Halmashauri kuhakikisha kila idara zote katika Halmashsuri yake zinakuwa na vitabu vya Irani ya chama ili kuwa na Dira ya utekelezaji wa Miradi yake ili kuwa na uhakika wa miradi yote iliyo ainishwa kwenye irani hiyo ili itakapo fikia kipindi kilicho pangwa ikamilike kwa wakati.

Katika taarifa hiyo Katibu akatumia nafasi hiyo kuwaagiza Wataalamu kuzingatia utoaji wa ajira za watu watakao tumika katika shughuli za uandikishaji wa zoezi la Sensa ya watu na makazi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi wilaya ya Tunduru Mustafa Bora

Akatumia nafasi hiyo kuwataka Wananchi kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya watu na makazi inayo tarajiwa kufanyika Agost 23  Mwaka huu.

Awali Mratibu wa sensa ya watu na makazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Enock Kabakaki alisema kuwa tayari zoezi hilo limepangwa kufanyika kidijitali lipo tayali kupitia ofisi ya Takwimu za Taifa  imeandaa Madodoso 4 ya msingi kwa  jamii, majengo au nyumba na makazi zitakazo tumika kwa ajili ya utekelezaji wa zoezi hilo.

Kabakaki aliendelea kufafanua kuwa hadi sasa tayari wameanza kubainisha na kutenga maeneo 1,176 ambayo yatatumika kwa ajili ya kuhesabiwa pamoja na kuunda kamati za wilaya, Vijiji , vitongoji  na kwamba pia hadi sasa zoezi la  usajili wa anuani za makazi limefanywa  kwa asilimia 102.

Akitoa salamu za serikali kwa niaba ya  Mkuu wa wilaya ya Tunduru Julius mtatiro , kaimu afisa tawala wa Wilaya Augustino Maneno pamoja na mambo mengine aliwataka madiwani kuendelea kutoa elimu na maelekezo ya namna zoezi hilo la sensa  litakavyofanikiwa.

“Wote tunajua kilicho jitokeza katika awamu ya sensa iliyopita hivyo kila kiongozi inafaa ajipange na kulifanya zoezi hilo kuwa agenda ya kudumu katika vikao vyetu” alisisitiza Maneno na kuongeza kuwa hiyo iwe chachu ya mabadiliko katika jamii yetu ili kufikia malengo.

Sambamba na maelekezo hayo pia akatumia nafasi hiyo kwa kuwataka madiwani hao kuwaelekeza wananchi wao juu ya utekelezaji wa zoezi la uwekaji wa anuani za makazi katika makazi yao lililopo mbele yao.

Aidha  maneno pia aliwataka wanafamilia  kutunza chakula baada ya msimu wa mavuno ili kujiondoa kwenye adha ya upungufu wa chakula endapo unaweza kutokea mbeleni.

Kuhusu utekelezaji wa miradi inayo tolewa na Serikali ikiwemo ya ujenzi wa miradi ya ujenzi wa shule za Sekondari na Vituo vya Afya  katika kata za  Majimaji, Lukubule na Nakayaya kuwa imekuwa ina kusuasua sana utekekezaji wake hasa  kwenye upande wa nguvu za wanachi hali inayo onesha kuto kuwepo kwa maelekezo ya kutosha kwa viongozi wao.

Akitoa neno la shukurani Makamu mwenyekiti wa Halmashsuri ya Wilaya ya Tunduru Said Bwanali pamoja namambo mengine alisema madiwani wameyapokea maelekezo yote na kuahidi kuyafanyia kazi katika kipindi chao chote cha uwakirishi wao kwa wananchi.

Matangazo

  • MABADILIKO TAREHE YA USAILI TUNDURU DC June 22, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2022 HALMASHAURI YA WILAYA YA TUNDURU December 22, 2021
  • TANGAZO LA KAZI-Watendaji wa vijiji ,Madereva na Katibu Mahsusi May 20, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021 HALMASHAURI YA WILAYA YA TUNDURU December 19, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • DC MTATIRO AKABIDHI PIKIPIKI 64 KWA MAAFISA KILIMO TUNDURU

    June 24, 2022
  • KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI ROBO YA PILI

    May 02, 2022
  • MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA MUUNGANO

    April 27, 2022
  • MWENGE WA UHURU 2022

    April 11, 2022
  • Ona Zote

Video

KATIKA KUSHEREHEKEA UHURU WA TANGANYIKA.
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Taarifa ya Ukimwi kuishia decemba 2017
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.