• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

KIDODOMA kinara usimamizi wa Afya na Lishe robo ya kwanza 2023/2024.

Imewekwa : November 6th, 2023

Katibu Tawala Wilaya ya Tunduru Ndg. Milongo Sanga  ametoa cheti cha pongezi  kwa kata ya Kidodoma, ambayo imefanya vizuri katika usimamizi wa afya na lishe katika robo ya kwanza (Julai – Septemba 2023) , Novemba 06, 2023 katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru.

Halmashauri ya wilaya ya Tunduru imefanya kikao cha Tathmini ya utekelezaji wa  Mkataba wa afya za Lishe ngazi ya wilaya na jamii , Lengo ikiwa ni kuona mwenendo wa Lishe katika maeneo ya wilaya ya Tunduru, ili kujua hatua zipi ziendelee kuchuliwa kudhibiti viashiria vya Lishe kwa kipindi cha Robo ya kwanza (Julai – Septemba 2023) kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Ndg. Milongo Sanga ambaye ndiye alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho cha Tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa afya za lishe ngazi ya wilaya, kilichohudhuliwa na watendaji  kata wa wilaya ya Tunduru, Ndg Milongo Sanga aliwasisitiza Watendaji kuendelea  kusimamia masuala ya lishe kwani ni agenda ya kitaifa, kwa maeneo ambayo hayajafanyi vizuri zaidi kuendelea kusimamia viashiria hivyo nakuona vinafanya vizuri katika maeneo yao ya usimamizi.

Pichani ,Katibu Tawala Wilaya ya Tunduru Ndg. Milongo Sanga akizungumza katika kikao cha Tathmini ya Lishe robo ya kwanza, ambapo alikua Mwenyekiti wa kikao hicho.

“Lishe ni muhimu sana katika maeneo yetu kwani linachukuliwa kwa ngazi ya Taifa, kwahiyo watendaji twende tukasimamie viashiria vyote ili afya za wananchi wetu  zizidi kuimarika” Alisema.

Aidha kwa upande wake katibu wa kikao hicho cha Tathmini ya Lishe Ndg. Chiza Marando ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, amewataka watendaji kuzidi kuonesha ushirikiano kwa idara ya afya hasa katika sekta ya Lishe ili kuinua asilimia za usimamizi wa afya na Lishe katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.

Pichani, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Ndg. Chiza Marando (Aliesimama)  akizungumza wakati wa kikao cha Tathmini ya lishe, Ambapo alikua katibu wa kikao hicho.

Kitengo cha Lishe katika kuhakikisha inatatua changamoto nyingi za Lishe  inaendelea kuhamasisha viwanda vidogo vya  kuchakata chakula kuingia mikataba na SANKU kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa  virutubishi katika vyakula hivyo, pia kuhamasisha upatikanaji wa mbegu ziliongezwa virutubishi. SANKU ni wadau wa lishe ambao wanafanya Mradi wa uongezaji  virutubishi katika vyakula hasa  wakati wa uchakataji wa vyakula hivyo.

Pichani , baaadhi ya Watendaji wa kata zilizopo Wilaya ya Tunduru  Katika Kikao cha Tathmini ya Lishe Robo ya kwanza.

Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • SULUHU YA KUDUMU Maji Tunduru Yapatikana: Mkataba Wa Bilioni 3.2 Wasainiwa

    May 07, 2025
  • BODI Ya Wakurugenzi wa Mamlaka Ya Maji Na Usafi Wa Mazingira Tunduru (TUUWASA) Yazinduliwa

    May 07, 2025
  • TUNDURU Yajizatiti Kukabiliana na Ugonjwa wa Mpox.

    March 27, 2025
  • TUNDURU Yaungana katika Dua na Iftar

    March 24, 2025
  • Ona Zote

Video

WANANCHI WAENDELEA KUPATIWA MAFUNZO KWA VITENDO ILI KUTATUA MIGONGANO YA BINADAMU NA WANYAPORI.
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.