• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

Mfumo wa stakabadhi ghalani kuwanufaisha wakulima wa zao la ufuta.

Imewekwa : May 24th, 2019

Na Theresia Mallya-Tunduru

23/05/2019

Mnada wa kwanza wa zao la ufuta umeendeshwa leo wilayani Tunduru katika Tarafa ya Lukumbule ambapo jumla ya makampuni sita yalijitokeza kununua zao hilo na jumla ya Tani 239 sawa na kilogramu 239,000  zilinunuliwa na kampuni ya Sunshine limited ya dar es salaam  kwa bei ya shilingi 3080 kwa kilogramu moja.

Akifungua mnada wa ufuta Halmashauri ya Tunduru kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi.Christina Mndeme Mkurugenzi Mtendaji wilaya ya Tunduru Ndg.Gasper Zahoro Balyomi aliwapongeza wananchi wa wilaya ya Tunduru kukubali kuuza mazao katika vituo maalum kwa mfumo wa stakabadhi ghalani ili kumkomboa mwananchi kiuchumi.

Ndg.Gasper Balyomi aliwaambia wananchi wa wilaya ya Tunduru kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na viongozi wengine waziri mkuu na makamu wa rais wanawapongeza sana kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kwa kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na kulima mazao ya kimkakati kama Ufuta na Korosho.

Aidha alisema serikali imeanzisha mfumo huu stakabadhi ghalani  wa kuuza mazao katika vituo maalum kwa lengo la kila mwananchi kupata bei nzuri na kupambana na biashara za magendo zenye lengo la kumkandamiza mkulima.

Mkurugenzi huyo alifungua mnada wa kwanza Halmashauri ya Tunduru tarehe 23 mei 2019 uliofanyika katika kijiji cha lukumbule wilayani tunduru, huku akiwapondegza wananchi wa lukumbule kwa ushirikiano walioonesha kujitokeza kwa wingi katika mnada ambazo jumla ya Tani 239 sawa na kilogram 239,000 zitauzwa katika mnada wa hadhara.

Na kwa upande wake makamu mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika wilayani Tunduru ndg.Mussa Manjauli aliipongeza serikali kuitia bodi ya mazao mchanganyiko kuanzisha mfumo wa stakabadhi ghalani kwa zao la ufuta kwani utaongeza tija kwa wakulima.

Pia wakulima wa wilaya ya Tunduru watapata fursa ya kujiendeleza kiuchumi kwani kilimo kinachofanywa na wananchi wa tunduru kinategemeana wanapovuna ufuta na kuuza vizuri wanapata fedha kwa ajili ya kununua pembejeo za zao la Korosho.

“naipongeza serikali kwa kuweka usimamizi wa zao la Ufuta na kuingizwa katika mfumo wa stakabadhi ghalani kwani msimu wa kilimo uliopita wakulima waliuza holela na kupata kiasi cha shilingi 2300 kwa kilo lakini katika msimu tunaona matunda  makubwa kwani mnada wa kwanza  tuu umeanza kwa shilingi 3080 na kujitokeza kwa wanunuzi wenye uhakika ukilinganisha na huko nyuma” alisema Ndg Mussa Manjauli Makamu Mwenyekiti wa TAMCU.

Wananchi wa Lukumbule waliishukuru serikali kusimamia vizuri zao hilo na kuhakikisha kuwa mkulima anapata tija kwa kazi anazofanya, huku wakioomba serikali kusimamia katika malipo ili yafanyike kwa wakati kwani wengi wanategemea fedha za ufuta kwa ajili ya kununua viatilifu vya Korosho.

Bw.Mussa Amuri Chama “alisema mwaka jana ufuta uliuzwa kwa bei ya shilingi 2300 lakini sasa hivi tumeuza kwenye mnada shilingi ufuta ni shilingi 3080 tunaipongeza serikali kwa kweli lakini tuaomba maboresho yafanyike katika upatakanaji wa mbegu za kisasa na pembejeo kwa wakati”

Wananchi wengi wanafanya kilimo cha mazao kama sehemu ya chakula lakini ili kuendana na sera ya serikali ya kuinua uchumi wqa wananchi hadi kufikia kipato cha kati ifikapo 2025 imeamua kuweka nguvu katika usimamizi wa kilimo ili kiwe na tija kwa wakulima.

Mwisho

Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE Tunduru Yajadili Mikakati Ya Kuimarisha Afua Za Lishe Katika Jamii.

    November 13, 2025
  • DC MASANJA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MRADI WA MAJI MSINJI, ATAKA UKAMILISHWE HARAKA

    October 24, 2025
  • DC MASANJA ATOA WITO WA AMANI KWENYE UCHAGUZI, AENDELEA KUPIGA VITA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI TUNDURU.

    October 23, 2025
  • DC MASANJA AFANYA KIKAO NA TANAPA KUJADILI MIKAKATI YA KUIMARISHA MASUALA YA UHIFADHI TUNDURU.

    October 22, 2025
  • Ona Zote

Video

RC RUVUMA AWAPA POLE WANANCHI AMBAO NI MAJERUHI WA MGOGORO BAINA YA WAFUGAJI NA WAKULIMA TUNDURU
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.