• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

KAMPENI, kupinga ukatili wa kijinsia.

Imewekwa : November 25th, 2023

Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imefanya uzinduzi wa Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Nchini kuanzia Tarehe 25 Novemba hadi 10 Disemba 2023.

Katibu tawala Wilaya ya Tunduru Ndg.Milongo Sanga alikuwa Mgeni rasmi akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Tunduru. Uzinduzi huo umefanyika  katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, ambapo aliwasihi wadau kuendelea kuwa Mabarozi wazuri katika kupinga ukatili katika jamii, pia kutoa taarifa kwenye vyombo vya sheria vitendo vyote vya  ukatili kwa mamlaka zinahusika na kudhibiti ukatili wa kijinsia.

Aidha, Katibu Tawala amesema katika kutimiza  lengo la kampeni  hiyo, juu ya kupinga  vitendo vya ukatili katika jamii, yapaswa kuzingatia na  kuungana na asasi za kijamii katika kuelimisha, kuhamasisha,kukemea na kuchukua hatua kwa pamoja ili kupinga ukatili wa jinsia katika jamii.

"Tukiyazingatia haya,ni hakika kabisa ukatili katika jamii zetu, wilaya na Taifa kwa ujumla utapungua kwa kiasi kikubwa"

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Tunduru Bi.Brandina Sekela alizungumza kuhusu muongozo wa kampeni hiyo ya siku 16 katika kupinga ukatili,ambapo amesema lengo kuu la kampeni hii ni kuungana na wadau, kupata nguvu ya pamoja katika kuhimiza na kushawishi jamii kutokomeza vitendo vya ukatili wa jinsia ili kufikia usawa wa kijinsia.

Sambamba nae Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii  Bi. Letesia Mwageni,amezungumza juu ya shughuli zilizofanywa na Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru katika kuendelea kupinga ukatili wa kijinsia katika Jamii, hasa kwa kundi la wanawake ambalo lipo katika hatari kubwa ya kunyanyasika.

Kampeni hiyo imezinduliwa  Novemba 25 katika Mkoa wa Dar es salaam, na kilele chake kitakua Disemba 10, 2023, aidha kampeni hiyo inatakiwa kufanyika katika ngazi zote  kuanzia ngazi ya Vijiji/Mtaa, Kata na Halmashauri , ambapo Kauli mbiu ya  mwaka huu inasema "WEKEZA: Kuzuia Ukatili wa kijinsia".


Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • SULUHU YA KUDUMU Maji Tunduru Yapatikana: Mkataba Wa Bilioni 3.2 Wasainiwa

    May 07, 2025
  • BODI Ya Wakurugenzi wa Mamlaka Ya Maji Na Usafi Wa Mazingira Tunduru (TUUWASA) Yazinduliwa

    May 07, 2025
  • TUNDURU Yajizatiti Kukabiliana na Ugonjwa wa Mpox.

    March 27, 2025
  • TUNDURU Yaungana katika Dua na Iftar

    March 24, 2025
  • Ona Zote

Video

WANANCHI WAENDELEA KUPATIWA MAFUNZO KWA VITENDO ILI KUTATUA MIGONGANO YA BINADAMU NA WANYAPORI.
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.