• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

Kamati ya ujenzi wa Bwalo Nandembo sekondari watakiwa kutekeleza Majukumu yao.

Imewekwa : June 12th, 2019

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tunduru Gasper Zahoro Balyomi wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa bwalo la chakula linalojengwa katika shule ya sekondari ya Nandembo iliyopo wilayani Tunduru

Serikali imetoa jumla ya shilingi Milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa Bwalo la chakula na Ukumbi wa Mikutano katika shule ya Sekondari Nandembo yenye kidato cha kwanza hadi sita,mradi uliotakiwa kukamilika tangu Mwezi Mei,hata hivyo hadi sasa ujenzi huo haujakamilika na huko katika hatua ya msingi jambo linalo leta  wasiwasi kama kazi hiyo inaweza kumalizika.

Wakizungumza kwa niaba ya wenzao ,baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo Rashid Ali na Bashiru Yacob wamesema, kwa sasa wanapata tabu kubwa kila  unapofika muda wa chakula na wanatumia   miti iliyopo shuleni hapo  jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa maisha yao.

Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi Christopher Simkoko akimuonesha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tunduru Gaspar Balyomi ujenzi wa Bwalo la chakula na ukumbi wa mikutano unaojengwa katika shule ya sekondari Nandembo

Aidha,wamemuomba fundi aliyepewa jukumu hilo kuhakikisha anaongeza kasi ya ujenzi ili likamilike kwa wakati ili wanafunzi wapate sehemu nzuri na salama kwa ajili ya chakula na hata ukumbi wa mikutano.

Bashiru Yacob alisema, kula chakula chini ya miti ni hatari kwani wanaweza kupata vimelea vya magonjwa mbalimbali kama Tumbo na kuharisha kutokana na uzembe unaofanywa na fundi aliyekabidhiwa kazi ya ujenzi wa mradi huo.

Kwa upande wake,Mkuu wa shule hiyo ambaye ni katibu wa  kamati ya ujenzi Mwalimu Mary Ndunguru alisema, wamepokea shilingi Milioni 100 kwa ajili ya  mradi wa Bwalo na ukumbi wa mikutano hata hivyo  ambapo mradi huo ulitakiwa kukamilika mwishoni mwa  mwezi Mei,lakini umechelewa kukamilika kwa muda muafaka kutokana na mifumo ya fedha na fundi kushindwa kufanya kazi yake kwa wakati.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Komred Gaspar Balyomi akikagua ujenzi wa Bwalo la chakula na Ukumbi wa Mikutano unaojengwa katika Shule ya Sekondari Nandembo wilayani Tunduru,hata hivyo ujenzi huo uliotakiwa kukamilika Mwezi Mei Mwaka huu upo katika hatua ya msingi kutokana na fundi wake kushindwa kukamilisha kazi hiyo kama ilivyokusudiwa.

Alisema, hadi sasa wametumia shilingi milioni 17 kati ya shilingi Milioni 100 na fedha zilizobaki  shilingi milioni 83 ambazo ziko Benki,  hata hivyo kuchelewa kukamilika kumewaathiri sana wanafunzi wake ambao wanatumia kivuli cha miti kwa ajili ya kulia chakula na kufanya mikutano ya kitaaluma. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Gaspar Balyomi akiwa katika eneo la mradi huo ametoa maagizo ya mradi huo kukamilika ndani ya mwezi mmoja kwa kuzingatia ubora na viwango.

 Gasper alisema "natoa siku thelathini mradi kwa fundi Keneth John mradi huu uwe umekamilika, naomba mfanye  kazi usiku na mchana ili kumaliza kazi hiyo"

Alisema, mradi huo huko nyuma kwa asilimia 50 na kuna uzembe mkubwa umefanyika katika usimamizi wake na ameitaka kamati ya ujenzi kuhakikisha inapeleka vifaa vyote vinavyohitajika  ili kazi iende haraka na wanafunzi waondokane na  kero kula chakula chini ya miti..

MWISHO

Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • SULUHU YA KUDUMU Maji Tunduru Yapatikana: Mkataba Wa Bilioni 3.2 Wasainiwa

    May 07, 2025
  • BODI Ya Wakurugenzi wa Mamlaka Ya Maji Na Usafi Wa Mazingira Tunduru (TUUWASA) Yazinduliwa

    May 07, 2025
  • TUNDURU Yajizatiti Kukabiliana na Ugonjwa wa Mpox.

    March 27, 2025
  • TUNDURU Yaungana katika Dua na Iftar

    March 24, 2025
  • Ona Zote

Video

WANANCHI WAENDELEA KUPATIWA MAFUNZO KWA VITENDO ILI KUTATUA MIGONGANO YA BINADAMU NA WANYAPORI.
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.