Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mh Mbwana Mkwanda Sudi katika mahafali ya pili ya kidato cha sita katika shule ya sekondari ya wasichana Masonya yaliyofanyika katika viwanja vya shule hiyo mapema wiki,shule ya sekondari Masonya ilianzishwa mwaka 1994 chini jumuiya ya wazazi na mwaka 2014 shule ilianza kupokea wananfunzi wa kidato cha tano kwa michepuo ya GHL na HGK na kwa mwaka 2017 ina jumla ya wahitimu wapatao 39 ambao 19 ni mchepuo wa HGK na 20 ni HGL.
Akisoma taarifa kwa mgeni rasmi Mh Mbwana Mkwanda Sudi wakati wa sherehe za mahafali mkuu wa Shule ya wasichana Masonya Bi Elice Banda alisema shule ya wasichana masonya katika matokeo ya mwaka 2016 ilishika nafasi ya kwanza kimkoa, hivyo ni vyema wahitimu kuongeza bidii na kuhakikisha historia nzuri inaendelea.
Elice Banda alisema pamoja na mafanikio waliyopata katika taaluma bado wanakabiliwa na changamoto za ukosefu wa walimu hasa wa masomo ya sanyansi na baadhi ya masomo ya sanaaa, pia shule ina miradi mbali mbali inayoendeshwa kwa ushirikiano wa walimu na wanafunzi katika dhana ya elimu ya kujitegemea na kujifunza stadi za maisha lakini pia kuongeza kipato cha shule na kumudu kulipa gharama za watumishi wa ajira za muda.
Akitoa hotuba kwa wahitimu , walezi, wazazi na wanafunzi wa shule ya wasichana masonya mgeni rasmi katika mahafali ya pili ya kidato cha Mh Mbwana Mkwanda Sudi ambaye pia ni mwenyekiti wa halmasahuri ya wilaya ya tunduru alianza kwa kushukuru uongozi wa shule , na wahitiumu kwa uvumilivu mkuu walionesha kwa kipindi chote cha masomo bila ya kukata tamaa.
Mh Mkwanda Sudi aliendelea kusema amekisikia kilio cha wanamasonya na serikali imepanga fedha za kutosha katika Bajeti za Halmashauri ili kuhakikisha wananboresha shule hiyo na kuboresha mazingira ya kusomea kwani inatambua umuhimu mkubwa wa shule na ina mchango mkubwa sana katika jamii.
Aidha aliendelea kawahusia wahitimu kuyashiki mafunzo yote walijifunza na kwenda kuyaishi na sio wanaenda kuwa mizigo kwa wazazi na jamii na wasikubali kumezwa na malimwengu kwani safari yao y aelimu bado inaendelea,
Mh mwanda Sudi alisema kuwa elimu ni bahari haina mwisho na kuwataka wahitimu kufikiria kusonga mbele zaidi katika elimu ya juu, na miongoni mwenu ndipo watatoka viongozi mbali mblali wa nchi yetu na sera ya serikali ya uchumi wa kati ifikapo 2015 itafanikiwa kwa asilimia kubwa kwa kuwekeza katika Elimu.
"Elimu ni msingi wa maisha msidanganyike na ya dunia, wananume wasiwadanganye muache kusoma mkaolewe, au wazazi wasiwe sababu ya kushindwa kufikia ndoto zenu,mtakuja kujuta baadaye" alisema Mh Mkwanda Sudi.
Hata hivyo wanafunzi wa kidato cha tano katika Igizo waliwakumbusha wazazi juu ya haki ya mtoto wa kike kupata elimu ni sawa na mtoto wa kiume na jamii ambazo hawamdhamini mtoto wa kike waone kuwa watoto wote ni sawa na wanastahili kupata haki sawa bila ya kujali jinsi zao,
Na wahitimu kutodanganyika ya duniani na kuona mwisho wa kusoma umefika wakati bado kuna safari nje ya darasani na kuna elimu baada ya kidato cha sita, ni wakati wa mtoto wa kike kuamka na kupata haki sawa na mtoto wa kiume.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.