Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Ndg. Chiza C. Marando, amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo.Ziara hii imeanza tarehe 25 Mei 2024 na inatarajiwa kumalizika tarehe 29 Mei 2024.
Katika ziara hii, Ndg Marando amekwisha tembelea tarafa mbili za Lukumbule na Nakapanya. Amekagua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa shule, zahanati na Vituo vvya Afya.
Ndg.Marando amewataka wasimamizi wa miradi hii kuhakikisha inakamilika kwa wakatina kwa ubora unaokubalika. Amesema miradi hii ni muhimu sana kwa wananchi waTunduru kwani itaboresha huduma za kijamii kama vile elimu, afya, na maji.
"Wasimamizi wa miradi hii hakikisheni inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaokubalika. Miradi hii ni muhimu sana kwa wananchi wetu na itabawa maendeleomakubwa katika Wilaya yetu," amesema Ndg. Marando.
Ndg.Marando ameambatana na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru katika ziara hii, akiwemo Wakuu wa Idara za manunuzi, idara ya Afya, Waandisi wa wilaya pamoja na Idara za Elimu. Amewataka wataalamu hawa kushirikiana kwa karibu ili kuhakikisha miradi hii inatekelezwa kwa ufanisi.
Ziara hii ya Mkurugenzi Mtendaji inaonyesha dhamira ya Halmashauri ya Wilaya yaTunduru ya kuleta maendeleo kwa wananchi wake. Inatarajiwa kuwa miradi hi iitakayokaguliwa itakamilika kwa wakati na itaanza kutoa huduma kwa wananchi hivi karibuni.
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.