• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maliasili na Utalii
      • Ushirika
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Mawasiliano Serikalini
      • Michezo,Utamaduni na Sanaa
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za Watumishi
    • Elimu
      • Elimu ya awali na elimu msingi
      • Elimu Sekondari
    • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

DC Homera aendesha harambee ya uchangiaji ujenzi madarasa katika shule ya Msingi Mindu.

Imewekwa : May 12th, 2019

Na Theresia mallya –Tunduru

12/05/2019

Katika kupunguza tatizo la wanafunzi kutembea umbali wa zaidi ya kilomita moja kutoka kijijini hadi shule ilipo wananchi wa kijiji cha Mindu kilichopo Halmashauri ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wazazi wameshiriki ujenzi wa vyumba 5 vya madarasa na ofisi ya walimu moja.

Akisoma taarifa ya Kata ya Mindu kwa mkuu wa wilaya Juma Zuberi Homera mtendaji wa Kata ya Mindu Ndg William Charles Mngwira alisema kuwa watoto wamekuwa wakitembea umbali wa zaidi ya kilomita moja kwenda shuleni hali inayohatarisha usalama wao  hasa wale wa darasa la awali na darasa la kwanza hadi tatu, na kwa watoto wa kike.

Kutokana na adha hiyo alisema kijiji cha Mindu kilichokuwa kikitumia shule  iliyotumika toka kipindi cha ukoloni iliyojengwa mwaka 1936 kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya upili, (Middle Class)  kumeleta changamoto kwa watoto kuwa na utoro wa rejareja, mahudhurio hafifu, baadhi ya watoto kuacha shule na kukosekana kwa usalama wa watoto.

Serikali ya kijiji kwa kushirikiana na wazazi wameamua kuanzisha ujenzi wa madarasa 5 kwa nguvukazi za wananchi na fedha iliyotumika ni shilingi 11,880,000/=, ambapo mbunge wa Tunduru Kaskazini Eng Ramo Makani alitoa mchango wa milioni 5.

Madarasa haya yaliyojengwa katika makazi ya wananchi yapo katika hatua ya kuezeka, ambapo jumla ya bati 270 zinahitajika ili kukamilisha ujenzi huo na  kuondokana na tatizo la watoto kutembea umbali mrefu kufata huduma ya elimu.

Aidha taarifa iliendelea kusema kuwa Kata hiyo yenye wakazi zaidi ya 7000 haina sekondari ya Kata hivyo kukamilika kwa ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi yaliyokaribu na makazi ya wananchi kutatoa fursa ya ukarabati wa majengo ya iliyokuwa shule ya msingi Mindu kuwa shule ya sekondari.

wananchi wa kijiji cha mindu wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera kwenye mkutano wa hadhara ambaye hayuko kwenye picha.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Tunduru Mhe. Juma Zuberi Homera alianza kuupongeza uongozi wa kata, kijiji, shule wananchi wote wa Kata  hiyo kuona umuhimu wa watoto wao na kuanzisha ujenzi  wa majengo ya shule ya msingi Mindu katika makazi ya kijiji kwani itaongeza morali kwa watoto kupenda shule zaidi.

Mkuu wa wilaya hiyo alisema kuwa ametembelea eneo la ujenzi na kuona kazi nzuri inayofanywa na wananchi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa,pia  alipata fursa ya kufika kwenye shule wanayosoma watoto kwa sasa ambayo ni mbali sana kutoka kijijini hadi kufika shuleni hivyo sio salama kwa watoto hasa wale wadogo wa madarasa ya chini.

“Nimeona  juhudi zenu katika kumaliza changamoto ya wanafunzi kutembe umbali mrefu kwa kujenga majengo ya shule ndani ya mazingira ya kijiji, na katika taarifa nimesikia kuna changamoto ya kumalizia ujenzi huo kwa kukosa fedha ya kununua bati”alisema mkuu wa wilaya.

Aidha Mhe.Juma Zuberi Homera  alipata fursa ya kuendesha harambee kwa wadau wa maendeleo wilayani Tunduru ili kupatikana kwa bati 270 zinazohitajika katika kuezeka majengo hayo ili yaanze kutumika hadi ifikapo disemba 2019.

Katika harambee hiyo iliyoendeshwa na mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera kwa wadau wa maendeleo wa wilaya ya Tunduru,wadau walitoa ahadi ya kuchangia bati 161  ikiwa ni pamoja na mkuu wa wilaya kuchangia Bati 55 kuunga mkono juhudi za wananchi.

muonekano wa vyumba vya madarasa yanayojengwa kwa nguvu za wananchi na mchango wa mfuko wa jimbo Tunduru kaskazini ili kuondoa changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda shuleni wanakosoma kwa sasa.

Juma Homera alisema “katika kata ya Mindu nimafanya mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na kutoa michango ya bati 5 za kueezeka matundu ya choo shule ya mingi Mtonya, saruji mifuko 50 shule ya msingi Mjimwema na fedha taslimu laki tano (500,000) shule ya msingi Liwangula lakini niwaombe wazazi wa Mindu kuwachangia watoto chakula shuleni ili watoto wasome kwa utulivu na kusoma katika mazingira rafiki”

Na kwa upande saimon Ambul Simbuya mkazi wa kijiji cha Mindu alisema kuwa watoto wanapata adha sana kutembea umbali mrefu kutoka kijijini kwenda shuleni ambapo hali hii hatari sana kwa watoto wadogo hasa kipindi cha mvua na ni raisi hata kukutana na wanyama wakali njiani.

Saimon simbuya alieleza kuwa kata yao ya Mindu haina shule ya sekondari hali inayoadhiri watoto wanaofaulu kutoka shule za kata hiyo kwenda shule ya kata jirani, hivyo kukamilika kwa majengo ya shule wanayojenga kutarahisha kwani watafanya ukarabati wa madarasa ya shule inayotumika kwa sasa kuanzisha shule ya sekondari.

“wanafunzi wengi wa kike wa sekondari kutoka Kata ya Mindu wanakatiza masomo kutokana na kwenda kusoma katika shule ya kata jirani sekondari ya Mtutura na kuishi mtaani kwa kujitegema hivyo hupata mimba na kuacha masomo, kuanzishwa kwa sekondari tutapunguza tatizo na kupata wasomi wengi katika kata yetu”alisema bw. Simbuya.

Naye mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mindu alisema kuwa kumekuwa na tatizo la utoro kwa wanafunzi hasa kipindi cha mvua unaochangiwa na umbali, wanafunzi kuchelewa shuleni na pia utoro unachangiwa kwa kiwango kikubwa na ukosefu wa chakula shuleni endapo watoto watakua wanapata chakula cha mchana shuleni tatizo hili litapungua.

Lakini uongozi wa shule uliona changamoto hiyo hivyo ikaamua kushirikiana na serikali ya kijiji  kujenga madarasa katika makazi ya kijiji ili kuondoa na kuamaliza kabisa tatizo hili na kujenga jamii yenye weledi kwani vijana wetu wakiacha shule wengi tutatengeneza taifa ambalo ni mbumbumbu na ile haki ya elimu kwa kila mtoto haitofikiwa.

Mkuu wa wilaya ya Tunduru amekuwa ni chachu kubwa sana katika kuchangia maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na maji, afya, elimu na nyingine ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma kwa wakati na kujikwamua kiuchumi na kufikia mafanikio ya maendeleo endelevu ifikapo 2025.

Matangazo

  • MKOPO WA HAZINA KWA WATUMISHI WA UMMA FUNGU 82N2 March 25, 2025
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA October 01, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA HADHARA December 12, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA WANAOTAKIWA KUSHIRIKI USAILI WA AJIRA YA MUDA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KATIKA WILAYA YA TUNDURU January 12, 2025
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • SULUHU YA KUDUMU Maji Tunduru Yapatikana: Mkataba Wa Bilioni 3.2 Wasainiwa

    May 07, 2025
  • BODI Ya Wakurugenzi wa Mamlaka Ya Maji Na Usafi Wa Mazingira Tunduru (TUUWASA) Yazinduliwa

    May 07, 2025
  • TUNDURU Yajizatiti Kukabiliana na Ugonjwa wa Mpox.

    March 27, 2025
  • TUNDURU Yaungana katika Dua na Iftar

    March 24, 2025
  • Ona Zote

Video

WANANCHI WAENDELEA KUPATIWA MAFUNZO KWA VITENDO ILI KUTATUA MIGONGANO YA BINADAMU NA WANYAPORI.
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.