IDARA YA MIFUGO NA UVUVI
Mkuu wa Idara Dk Eric Kahise
simu +255 765 293 627
UTANGULIZI
Idara ya Mifugo na Uvuvi ina jumla ya watumishi 24 na mkuu wa idara 1(mmoja), idara ya mifugo imegawanyika katika sekta mbili za Ufugaji na Uvuvi.
DIRA
Kuwe na sekta Mifugo ambapo ifikapo mwaka 2025 ambayo kwa sehemu kubwa itakuwa na ufugaji wa kisasa na endelevu,yenye mifugo bora ,yenye uzalishaji mzuri, inayoendeshwa kibiashara na yenye kuboresha lishe ya mtanzania, kuinua kipato cha mfugaji na Taifa na kuhifadhi mazingira
DHAMIRA
Kuhakikisha kuwa Rasilimali inaendelezwa na kutunzwa katika mazingira endelevu kwa ajili ya ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wananchi
MADHUMUNI
Kujenga sekta yenye ufanisi na ushindani ambayo itachangia kuboresha maisha ya wananchi ambao shughuli zao kubwa ni ufugaji na maisha yao hutegemea mifugo.
Sekta ya Mifugo inafanya Majukumu yafuatayo:
Sekta ya Mifugo ina sehemu tatu ambazo ni
Kazi za sekta ya uvuvi.
1. Hifadhi ya samaki, wanyama wengine wa majini na mazalia ya asili na kuandaa mazingira bora kwa vizazi vya sasa na baadae
2 Kuboresha njia za utoaji leseni za Uvuvi na maelekezo ya shughuli za uvuvi ili kuongeza kipato cha Taifa
3. Kuwezesha na kutekeleza Sheria na kanuni za Uvuvi kwa kufanya doria za mara kwa mara ili kuzuia Uvuvi Haramu kwenye mito na maziwa katika Wilaya ya Tunduru
4 Kutumia Rasilimali zilizopo ipasavyo ili kuongeza upatikanaji wa samaki na hatimaye kukuza Uchumi wa Taifa
5 Kuandaa na kufanya mafunzo kwa wavuvi
6 Kuwezesha na kusimamia hifadhi ya mazingira
7. Kuwezesha ukusanyaji takwimu za samaki na kipato
8. Kushirikisha Jinsi katika kuendeleza sekta ya Uvuvi
Halmashauri ya Wilaya Tunduru
Anuani ya Posta: 275, TUNDURU
Simu: + 255-025-2680004
Simu ya Nununu:
Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz
Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.