• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Tunduru District Council
Tunduru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Vision and Mission
  • Utawala
    • Departiment
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Msingi
      • Maji
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maliasili na Utalii
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Utumishi
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Information, Technology, Communication and Public Relation
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Biashara na Viwanda
    • Mining
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Huduma za Watumishi
    • Kilimo
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Mifugo na Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha za Madiwani
      • Kata ya Mbati
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Huduma za Jamii
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Time Table
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Tarajali
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa wateja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

Historia

HISTORIA YA WILAYA YA TUNDURU

Wilaya ya Tunduru ni miongoni mwa wilaya sita (6) za Mkoa wa Ruvuma. Wilaya hii ilianzishwa mwaka 1905 kipindi cha utawala wa ukoloni ambapo serikali ya Ujerumani ilijenga boma katika eneo la Kadewele karibu na lilipo jengo la Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa sasa.

 

UKUBWA WA WILAYA NA MAENEO YA KIUTAWALA

Wilaya ya Tunduru ina ukubwa wa kilometa za mraba 18,778. Pia, Wilaya ina Tarafa 7, Kata 39, Vijiji 157, Vitongoji 1,166 na Majimbo 2 ya Uchaguzi (Tunduru Kaskazini na Tunduru Kusini). Wilaya ina Waheshimiwa Madiwani 53 (Wakuchaguliwa 39, Viti Maalumu 14), na Waheshimiwa Wabunge 3 (Wakuchaguliwa 2 na Viti Maalum 1).

Wilaya ya Tunduru ipo kati ya nyuzi 36° 30’ na 38° Longitudo kuelekea upande wa Mashariki, nyuzi 10° 15’ na 11° 45’ Latitudo Kusini ya Ikweta.

  • Upande wa Kaskazini Wilaya ya Tunduru inapakana na Wilaya ya Liwale (Lindi).
  • Upande wa Magharibi inapakana na Wilaya ya Namtumbo.
  • Mashariki inapakana na Wilaya ya Nachingwea (Lindi) na Masasi (Mtwara).
  • Upande wa Kusini inapakana na Jamhuri ya Watu wa Msumbiji ambapo Mto Ruvuma hufanya mpaka wa kudumu kati ya nchi ya Tanzania na Msumbiji.

 

IDADI YA WATU

Kwa mujibu wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika Agosti, 2012 idadi ya wakazi ilikuwa 298,279 kati yao Wanaume ni 143,660 (48.2%) na Wanawake ni 154,619 (51.8%). Mwaka 2016, Wilaya inakadiriwa kuwa na wakazi 331,821 kati yao Wanaume ni 159,815 na Wanawake ni 172,006. Wastani wa ongezeko la wakazi katika Wilaya ya Tunduru ni asilimia 2.7 kwa mwaka.

 

HALI YA HEWA

Hali ya hewa ni ya joto la wastani wa nyuzijoto 25°c linalofaa kwa ustawishaji wa mazao mbalimbali. Wastani wa mvua ni milimita 960 kwa mwaka ambapo mvua hunyesha kuanzia mwishoni mwa mwezi Novemba hadi Aprili.   Aina ya uoto   ni miombo.  Hali ya udongo ni mchanga na mfinyanzi kwenye maeneo ya mabonde. Asilimia 30 ya vijiji ndani ya wilaya vina mito isiyokauka kwa mwaka mzima. Wilaya ya Tunduru ina mwinuko wa kati ya meta 200 na 500 kutoka usawa wa bahari na hali ya nchi ni ya tambarare na vilima upande wa Kusini Magharibi.

SHUGHULI ZA KIUCHUMI

wilaya ya Tunduru ni wilaya ambayo shughuli kubwa za kiuchumi ni kilimo cha zao la biashara la korosho ambayo hulimwa karibu katika maeneo yote ya wilaya, pia watu wa Tunduru wanalima mazao mengine kama mpunga, mbaazi, choroko, kunde,ufuta na karanga.

wilaya ya Tunduru ina vivutio mbalimbali vya utalii ambavyo ni mbuga ya wanyama selous, mapori ya akiba ya sasawala na muhuwesi, masalia ya majengo ya wapigania uhuru wa msumbiji kupitia chama cha Frelimo, makaburi ya viongozi wa kimila, Miti inayogeuka kuwa mawe, mapango ya ajabu na nyayo za wanyama katika mwamba vyote hivi ni sehemu ya utalii na vinapatikana katika wilaya ya Tunduru pekee.

shuguli nyingine za uchumi zinazofanywa na wananchi wa wilaya ya tunduru ni shughuli za biashara, ufugaji wa nyuki, kuku, samaki, mbuzi na ngombe. pia wanafanya biashara za aina mbalimbali katika mazingira yao.

MAKABILA.

Wilaya ya Tunduru wakazi wake ni kabila kubwa la wayao, na makabila mengine ni ngoni, makua, na wandendeule.

Utamaduni

kabila la wayao kama zilivyo jamii nyingi za mikoa ya kusini wakati wa mavuno wanakuwa na ngoma, na baada ya mavuno wengi wao huandaa sherehe za jadi maafu kama unyago. ngoma hii huwa na lengo la kuwafundisha mabinti namna ya kukabiliana na changamoto za maisha hasa katika ndoa. kuna aina mbali mbali za ngoma kama mabega, mganda nk.




Matangazo

  • Matokeo ya kidato cha Nne, QT, Kidato cha Pili, na Darasa la Nne January 17, 2021
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2022 HALMASHAURI YA WILAYA YA TUNDURU December 22, 2021
  • TANGAZO LA KAZI-Watendaji wa vijiji ,Madereva na Katibu Mahsusi May 20, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021 HALMASHAURI YA WILAYA YA TUNDURU December 19, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI ROBO YA PILI

    May 02, 2022
  • MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA MUUNGANO

    April 27, 2022
  • MWENGE WA UHURU 2022

    April 11, 2022
  • hafla ya upandaji miti

    March 31, 2022
  • Ona Zote

Video

KATIKA KUSHEREHEKEA UHURU WA TANGANYIKA.
Video Nyingine

viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA MITIHANI
  • Mkataba wa huduma kwa Mteja
  • muongozo wa Tehama
  • Ijue Sheria ya Umiliki wa Ardhi ya Mwaka 1999
  • Taarifa ya Ukimwi kuishia decemba 2017
  • Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Tunduru

Tovuti linganifu

  • Tovuti Kuu ya Rais - IKULU
  • Ofisi ya Rais - UTUMISHI
  • Ofisi ya Rais - TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

wasomaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya Tunduru

    Anuani ya Posta: 275, TUNDURU

    Simu: + 255-025-2680004

    Simu ya Nununu:

    Barua Pepe: info@tundurudc.go.tz

Anuani nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Kituo

Hakimiliki©2019 Halmashauri ya Wilaya Tunduru.Haki zote zimehifadhiwa.